MBONA HAJIONGEZI?   SEHEMU YA 03 na GASPER WA MASTORY

MBONA HAJIONGEZI?
  SEHEMU YA 03
na GASPER WA MASTORY
♡♡♡♡♡♡♡♡♡♡♡
ILIPOISHIA
brandon alimsogelea. vanessa na kumshka begani akawa yupo karibu. naye akamsogelea sikioni taratibu,vanessa mapigo ya moyo yakaanza kumwelemea...SONGA NAYO.....
vanessa mapigo ya moyo yakaanza kumwelemea akajua brandon maji yashamzidi unga naye hakufanya ajizi akaona kama ule wasaa wa tamanio la moyo wake kutimia akajisogeza karibu zaidi ili aruhusu kitakachotokea kitokee . brandon akamnong'oneza taratibu kwa sauti yake ya kiume "najua hujanielewa so jitahidi sasa uwepo hapa kimawazo dada yangu" baada. yakusema hayo brandon alijivuta mara moja na kukaa kwenye kiti na kushika peni akaanza. kushuka vitu. kwenye daftari.vannesa alighadhabika moyoni akidhani brandon labda atambusu au kumpa romance lakini haikuwa hivyo.aliona aibu kwa kujishaua kwake akaona bora amsikilize tu kwa makini. baada ya kumaliza kusoma brandon aliongeza juisi ya embe wakanywa pamoja kwa furaha..kwakuwa walikuwa wamechoka choka wakatoka mule ndani na kwenda kutembea tembea maeneo ya uwanja wa basket’ brandon alibeba mpira kabisa .akamwambia vannesa aende akabadilishe nguo avae za michezo ili akamfundishe mpira huo.vanessa alienda kubadili. na hazikupita dakika nyingi alirudi akiwa ndani ya vazi la track suit za rangi ya damu ya mzee ambazo zilimfit barabara mwili wake.
walianza kuondoka na kuelekea uwanjani  wakati wakiwa huko brandon alikuwa anamfundisha kucheza mpira huo wenye ladha ya aina yake vanessa ambaye alikuwa ameumbika si haba alikuwa amevaa nguo za heshima tu lakini kutokana na shepu yake yenye kila aina ya uchokozi ilimfanya nguo zake zote alizokuwa anazivaa zionekana hazina heshima,
hakika wanaume wengi walimsumbua sana vanessa kila. mtu akijaribu bahati yake.lakini wengi kati yao waliambulia chaga..wengne wakiishia kula tu kwa macho kila akatishapo.hakuonekana kuwa na mwanaume yeyote chuoni hapo kama mpenzi wake na wala hakumkubalia yeyote chuoni hapo kiukweli alikuwa mwanamke wa tofauti sana. siku hiyo watu walipata mshangao mkubwa sana. kumwona binti huyo akicheza mpira uwanjani..binti ambaye mara zote alioneana kuwa bize na mambo yake. watu kadhaa walio pita eneo lile waliukodolea macho mwili wa binti Yule kwa jinsi ulivyokuwa umejitenga vyema hakuna asiyeweza kushawishika,mikogo yake sasa alivyokuwa akiudundisha mpira ule na kukimbiakimbia kuelekea golini kulifanya tetemeko dogo kutokea maeneo ya ukanda wa ikweta. Hakuna aliyeshindwa kukili kuwa binti Yule alizaliwa akazalika na kama kuumbwa basi aliumbwa akaumbika sawasawa. ‘’brandon mi nmechoka bhana we unanifunga tu magoli’’ ‘’ah sa si ndo ukazane na wewe urudishe’’ ‘’bwana tutaendelea siku nyingine mimi leo basi,sichezi tena’’ Baada ya kucheza kwa muda wakaanza kuondoka taratibu huku wakipiga stori za hapa na pale ‘’leo nmeelewa vizuri sana yani ,nashukuru sana kwa muda wako nmefurahi sana sijui hata nikupe nini?’’ ‘’usijali,mimi hata ukitabasamu tu kwangu ni zawadi tosha’’ ‘’dah unamoyo wa kipekee kama hutojali, ninakuomnba wikiend hii twende sehemu tukapunge upepo’’
‘’okey tutazidi kuwasiliana ntaangalia kama ratiba zangu zitakuwa hazijanibana naweza nikaja ila kama ikiwa tofauti naomba uwe tayari kukubaliana na hali’’ ‘’sawa sawa haina shida’’ Walimaliza mazungumzo kisha wakaagana na kila mmoja akaenda upande wa hosteli yake.

****************************** *************** Siku zilizidi songa huku binti angel akizidi teseka kwa penzi zito alilokuwanalo juu ya kijana Brandon alijitahidi kuufata ushauri wa rafiki zake lakini aliambulia kuona tu aibu kwani hata familia aliyokuwa ametokea ilimlea kwa maadili ambayo kumtega au kumtongoza mwanaume ilikuwa mwiko kwao hivyo hakuwa na ujasiri wa kunyanyua kinywa chake kumwambia Brandon mambo yalivyo ndani ya moyo wake,aliishia tu kujichekeshachekesha pale akutanapo na kijana huyo. hakika uvumilivu ulikuwa ukielekea ukingoni basi aliamua jambo moja.siku moja akiwa mjini akifanya manunuzi madogodogo wazo likamjia anunue zawadi yoyote kwaajili ya Brandon,kulikuwa na vitu mbalimbali ambavyo vilikuwa akilini mwake vyote alitamani anunue kama zawadi kwa ajiili ya Brandon . ‘’mmmh boksa, sio atanifikilia vibaya.ah! hapana sitamnunulia boksa kwanza siijui size ya kiuno chake’’ alijiwazia mrembo Yule ambaye alikuwa mrefu kwa kimo na mweupe kwa rangi mwenye asili ya kabila la kinyaturu aliumbika lakini sio kwa fujo kama ilivyokuwa kwa Vanessa yeye alikuwa na shepu ya kawaida tu ila iliyovutia kama miss flani hivi jambo la upekee kwake iliuwa ni mwendo wake,alitembea kwa aina yake yani ukiwa humjui unaweza dhani anafanya maksudi kumbe ndo alivyo,alitembea kama miss wanaoopita katika zuria jekundu wakati wa maonesho yao ya umiss,sauti nayo alijaliwa si haba yani utadhani mwanadada mwimbaji anayejiita African princes almaarufu kama nandy.

Basi wazo lilipita kuwa amnunulie zawadi Fulani ya pekee,baada ya kuinunua alimalizia mambo yake mjini huko na kurudi chuoni kisha akajiandaa tayari kwenda katika hosteli ya wavulana ambayo haikuwa mbali na hapo ,alijiremba kiasi kisha akavaa gauni flani ambalo halikuwa refu sana wala fupi sana lakini liliweza kuonesha sehemu kubwa ya mguu wake mweupe na wakuvutia,hakutumia muda mwingi kujiandaa akawa ameshamaliza na kabla hayaondoka akampigia simu Brandon. ‘’haloow Brandon ….’’
‘’halow mambo vipi?’’
‘’safi tu uko wapi saivi?’’ ‘’nipo zangu hostel nmepumzika’’ ..anhaaa samahani naweza nikaja’’ ‘’am okey unaweza kuja karibu’’
‘’okey sawa’’ alimaliza kuongea angel na kukata simu akafungua mlango na kuanza safari kwenda kwa Brandon .

Ngo ngo ngo ngo!! Mlango ulisikika ukigongwa, Brandon liinuka na kisha kwenda kuufungua...ITAENDELEA........ah mimi leo staki kusema sana ila akipona mtu humo ndani mimi nipo.......Nenda kalike page yangu inaitwa simulizi tamu za gasper kwa story nyingine tamu.

LihatTutupKomentar