KMC YATOA ANGALIZO KWA YANGA


Uongozi wa timu ya KMC umewataka mashabiki waungane leo uwanja wa taifa kushuhudia namna watakavyoiangusha Yanga kwa kuchukua Point tatu muhimu.

Ofisa habari wa KMC Anwar Binde amesema wanajua Yanga imekuwa na mwanzo mzuri baada ya kucheza michezo saba bila kupoteza mchezo hata mmoja hilo haliwapi shida kwa kuwa mpira unachezwa uwanjani.

"Ushindani upo, ila nina imani na kikosi chetu kwa kuwa maandalizi yamefanyika vizuri, wachezaji wana morali kubwa wanahitaji ushindi hicho ndicho tutakachokifanya mashabiki wajitokeze kwa wingi kuona tukifanya makubwa," alisema.

KMC imepanda daraja msimu huu imecheza michezo 10 na kushinda mchezo mmoja imepoteza michezo miwili na kutoa sare michezo saba ikiwa na pointi 10 inakutana leo na Yanga yenye jumla ya point 19 ambayo haijapoteza mchezo mpaka sasa.

LihatTutupKomentar