SIMULIZI;UCHAWI WA MAMA.
MTUNZI;RAJA SAIDY.
WHATSAPP;0756920739.
SEHEMU YA NANE
ILIPOISHIA.............
nachokushauli mkuu mi nina dawa nimeitoa zimbabwe huko ndo inapatikana tu kazi yake ni kuzuia mizimu sa cha msingi we ichukue iweke kwenye maji kisha uanze kumwaga hayo maji yake kwa kila mlango wa humu ndani.kazi hii ifanye kabla hata wanao hawajarudi,baada ya hapo kama walikuwa na mzimu utashindwa kuingia ndani utakuwa unaishia nje hivyo utakifanya kila unachokitaka"
"ahsante sana mshilika ndo maana nawategemea,si mnajua mi sina muda maalumu wa kazi ngoja nianze kuiweka hi dawa ili ianze kufanya kazi kabla hawajaja
je nini kitaendelea................
ENDELEA NAYO....................
***********
mapambano zidi ya babu yake nadya na wachawi wa mama yake nadya yalianza baada ya babu yake nadya kukasirishwa na tukio zima la wachawi wa mama yake nadya kumchukua mke wake, mkuu yule wa wachawi alijibadilisha na kuwa nyoka baada ya kuona babu yake nadya amejibadilisha na kuwa fisi,walianza kushambuliana kama wanyama poli,nyoka ambaye ni yule mkuu wa wachawi alianza kwa kumrushia sumu machoni ili fisi ambaye ni babu yake nadya asipate kuona vizuri ila kutokana na nguvu alizokuwa nazo babu yake nadya hivyo sumu hiyo haikumdhulu hata kidogo.fisi yule alimfuata nyoka kisha akamng'ata shingoni na kuanza kumgalagaza mithili ya mtu aliyefungwa na kamba huku akiendelea kuvutwa na gari,kutokana na ujuzi hule ulimfanya nyoka yule kuishiwa nguvu kisha akabadilika na kuwa mkuu yule wa wachawi kisha akaamua kumuomba msamaha babu yake nadya na kuhaidi atampa mke wake.babu yake nadya alibadilika na kuwa binadamu wa kawaida kisha akaomba mke wake aje muda huo la sivyo atamuuwa na hana huwezo wa kumtoroka.
Mchawi yule bila kubisha aliongea kwa sauti iliyo juu kwa maneno ya kichawi ,ghafla walikuja wachawi huku wakiwa wamemshikilia mke wa babu yake nadya ambaye ni bibi yake nadya.
Mchawi yule mkuu ambaye tayari alikuwa na majeraha yaliyokuwa yakionekana vyema katika sehemu mbali mbali.za mwili wake kutokana na kuwa alikuwa uchi wa mnayama, na pia muda sio mrefu alikuwa na pambano baina yale na babu yake nadya.wachawi wale waliweza kutii amri kisha wakamrudisha bibi yake nadya bila ya kumdhulu na kitu chochote kisha wakaondoka.
baada ya kuwa wameondoka babu yake nadya aligeuka na kuanza kumkagua mke wake ambaye alionekana bado kuwa katika hali ya usingizi,kutokana na kuwa tayari palikuwa pameshaanza kukucha hivyo alihitaji kumuamsha cha ajabu alijaribu kila anavyoweza lakini mke wake hakuitika"
babu nadya aliweza kuchukua begi lake kisha akaingiza mkono na kuchomoa kopo kubwa lililokuwa na dawa iliyokuwa na rangi nyeupe kisha akamimina ule unganga kwenye kiganja na kuupaka machoni ,hakuamini macho yake baada kukuta kumbe wachawi walikuwa wamemletea gogo na sio mke wake.
***************
nikiwa naendelea kushangaa sana maneno yale yaliyotoka kwa baba na kuniacha mdomo wazi mimi pamoja na mdogo wangu itakueje mzimu wa baba ututokee ama kweli tunashinda tunashida hasa ya kupambana na mama yetu mwenye roho ya paka ndani yake,hayo yote yalikuwa ni mawazo yangu baada ya kuwa muda si mrefu baba ametoka kuzungumza na sisi.
"caro mbona unawaza sana???"
"Dada kutokana na maneno ya baba nahisi kuchanganyikiwa naogopa hata kwenda nyumbani!!!!"
"kwa nini mdogo wangu unaogopa???"
"Dada nadya kama mama aliweza kula nyama ya baba mume wake wa ndoa,je kwa upande wetu ambao alituzaa wenyewe si huko kutukaanga kabisa.hicho ndio kinafanya niogope hata kwenda nyumbani"
"cha msingi basi kama huitaji kwenda nyumbani tutatafuta pa kukaa,nimefanya hivyo kwakuwa nimesikia maneno ya baba anatumia njia nyingi kutusaidia huwezi jua tukio lililopo kule nyumbani labda ametumia njia hiyo kutusaidia!!!!!"
"Ndio dada nadya huwezi jua"
"Basi sawa ngoja niongee na daktari atupe ruhusa ya kuondoka hapa"
"sawa mi nipo nakusubili"
niliweza kuondoka na kumuacha mdogo wangu caro kisha nikaelekea kwa daktari,nilipokea maelekezo ya daktari pia akatupa dawa za maumivu endapo mdogo wangu akisikia maumivu yoyote basi dawa zile zinakuwa msaada mkuu kwake.
Tuliondoka tukiwa na caro moja kwa moja,nikaelekea kwa rafiki yangu kipenzi judithi tuliyekuwa tunafanya naye kazi pale ofisini kwake hakukuwa mbali na hospitalini hapo hivyo tuliweza kuchukua dakika kumi kisha tukawa tumefika
"hodi,hodi,"
"nani??"
"judithi ni mimi nadya"
"Nadya??"
judithi aliongea kwa mshituko uliofanya akaja kufungua mlango kwa pupa,
"ooh my friend ulikuwa umepotelea wapi hata kazini hauji???"
"mmmh judithi rafiki yangu siku ngapi ngapi hizo hebu nipokee kwanza mwenzako nina shida hunioni hata nina mdogo wangu nina shida nipokee kwanza"
"haya ingieni ndani basi"
wakati tukiwa tumefika ndani kwa judithi ghafla mzimu wa baba ulitutokea kisha ukaanza kutusihi kwa ishara tusiweze kuingia ndani mwa judithi...........
je nini kitaendelea....................