AL AHLY WAICHAPA ESPERANCE 3-1 FAINALI YA KWANZA LIGI YA MABINGWA AFRIKA


TIMU ya Al Ahly ya Misri jana imetumia vyema nafasi ya kucheza nyumbani, baada ya kuichapa mabao 3-1 Esperance ya Tunisia katika fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria.
Kwa ushindi huo, Ahly ni kama wameweka mkono mmoja kwenye taji la tisa la rekodi la Ligi ya Mabingwa Afrika, kwani sasa watahitaji sare au kufungwa kwa tofauti ya bao moja tu katika mchezo wa marudiano Novemba 9 mjini Tunis ili kutwaa tena Kombe hilo.
Walid Soliman alifunga mabao mawili dakika za 34 na 76 na lingine Amr El Sulya dakika ya 58 upande wa Mashetani Wekundu wa Cairo, wakati bao pekee la Esperance lilifungwa na Youcef Belaili dakika ya 64.

Esperance watahitaji ushindi wa 2-0 kwenye mchezo wa marudiano Ijumaa ijayo Uwanja wa Olimpiki mjini Rades kutwaa taji hilo.
Kikosi cha Al Ahly kilikuwa; El Shenawy, Fathi/El Demerdash dk22, Samir, Coulibaly, Ashraf, Ashour, El Sulya, Hamoudi/Hussein dk67, Soliman, Mohareb na Azaro.
Esperance; Cherifia; Dhaouadi, Badri, Belaili, Chemmam, Coulibaly, Derbali, Chaalali, Erbeia, Khenissi/Mejri dk79 na Kom.

LihatTutupKomentar