--
From: Moses Francis mosesfrancis1790@gmail.com
MOSES FRANCIS
Huenda kuna wadau pamoja na mashabiki wa klabu ya Simba Sports Club wamekuwa wakiishangilia pamoja na kuiunga mkono timu yao lakini wakawa hawaifahamu vizuri histori ya timu yao. Makala hii inakuletea historia fupi ya klabu ya Simba tangu kuanzishwa kwake hadi sasa.
Simba Sports Club ni timu ya mpira wa miguu inayopatikana nchini Tanzania katika mitaa ya msimbazi, kariakoo inayopatikana katika jiji la Dar-es-salaam. Simba Sports Club imeanzishwa mwaka 1936, ni miaka takribani 82 tangu kuanzishwa kwa wekundu hao wa msimbazi. Tangu kuanzishwa kwake klabu ya Simba imepitia majina tofauti tofauti kwa nyakati tofauti tofauti. Kwa mfano klabu ya Simba ilikuwa inajulikana kwa majina tofauti tofauti kama vile Queens, Eagles, Sunderland kabla ya kupewa jina la Simba Sports Club ilipofika mwaka 1971 jina ambalo linatumika hadi sasa.
Klabu ya Simba imekuwa ikikabiliwa na upinzani mkubwa katika soka la Tanzania kutoka kwa mahasimu wao klabu ya Yanga, klabu ambayo ilianzishwa mwaka 1935 mwaka mmoja kabla ya kuanzishwa kwa klabu ya Simba Sports Club. Timu hizi pindi zinapokutana katika ligi kuu Tanzania bara pamoja na michuano mingine, mechi huonekana kuteka hisia wadau wa soka pamoja na mashabiki wanaoshabikia timu hizi zinazotoka mitaa ya kariakoo jijini Dar-es-salaam.
MAFANIKIO MECHI ZA KIMATAIFA
Miongoni mwa mafanikio makubwa ya klabu ya Simba ni pamoja na kufanikiwa kucheza fainali ya klabu bingwa ya kombe la shirikisho mwaka 1993 dhidi ya klabu ya Stella Club A'Adjame ya nchini Ivory Coast ambapo klabu ya Simba ilipoteza pambano hilo katika uwanja wa uhuru uliopo jijini Dar-es-salaam kwa kufungwa jumla ya magoli 2-0.
Mafanikio mengine makubwa ambayo klabu ya Simba imeyapata ni pamoja na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika yaliyofanyika mwaka 2003. Wekundu hao wa msimbazi walifanikiwa kuitoa timu ngumu ya Zamalek ya nchini Misri katika hatua ya mikwaju ya penati huku mchezaji bora wa mechi hiyo alichaguliwa kuwa ni golikipa wa klabu ya Simba Juma Kaseja ambaye alifanikiwa kucheza penati mbili dhidi ya mafarao hao wa Misri.
UBINGWA WA TANZANIA BARA
Tangu kuanzishwa kwake hadi sasa klabu ya Simba imefanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzani bara mara 19. Wekundu hao wa msimbazi wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu kwa nyakati tofauti tofauti ambapo wametwaa kombe hilo mnamo mwaka 1965,1966,1972,1973,1976,1977,1978,1979,1980,1993,1994,1994,1994,1995,2001,2002,2004,2007,2009,2011 na 2018.
KOMBE LA TUSKER
Klabu ya Simba imefanikiwa kutwaa kombe la Tusker kwa nyakati tofauti tofauti ambapo imetwaa kombe hilo mara 5. Wekundu hao wa msimbazi maarufu kama mnyama imetwaa kombe la Tusker mwaka 2001, 2002,2003,200 na 2005.
MAFANIKIO MENGINE
Ukiachana na inshu ya ya makombe klabu ya Simba imekuwa ni timu ya kwanza nchini Tanzania kuamua kujiendesha yenyewe chini ya mwanahisa mfanyabiashara bilionea Mohamed Dewj Mo' ambaye anamiliki hisa zipatazo asilimia 50 katika klabu hiyo mpaka sasa. Hiyo ni historia fupi inayoihusu klabu ya Simba tangu kuanzishwa kwake mpaka sasa. Napenda kuhitimisha kwa kuitakia uchaguzi mwema klabu ya Simba Sports Club uchaguzi ambao unatarajia kufanyika siku ya leo. Ahsante.