SIMULIZI;UCHAWI WA MAMA. MTUNZI;RAJA SAIDY. WHATSAPP;0756920739

SIMULIZI;UCHAWI WA MAMA.
MTUNZI;RAJA SAIDY.
WHATSAPP;0756920739.

SEHEMU YA PILI

ILIPOISHIA...........

nilivyomaliza kuongea hivyo baba alipotea katika eneo lile huku mama akiendelea kunikazia macho wakati akiwa pale pale kitandani,
"mwanangu nadya baba yako kaishafariki,mimi ndo nimemuuwa mwili wake huko hapa kitandani ule uliyokuwa unauona ulikua mzimu wake tu"
  je nini kitaendelea........

ENDELEA NAYO..........

"Mama kwanini umemuuwa baba?amekukosea nini eeh si nakuuliza si nakuuliza"
  niliongea kwa uchungu na hasira huku nikiendelea kumtazama mama aliyoonekana kutokuwa na wasiwasi hata kidogo.
"mwanangu nadya hicho kiherehere chako nitakuondoa duniani we nichefue,nakupa onyo la mwisho kaa kimya"
"sikai mama siwezi kukaa kimya kwa kifo cha baba yangu hata siwezi,niuwe na mimi niuwe mama"

mama tayari alikuwa kaishapandwa na hasira bila kuniongelesha kitu chochote kile.aliinua godoro lake kisha akachukua kikopo kidogo cha mafuta na kuanza kukifungua,ndani ya kijikopo hicho kulikuwa  na ungaunga mweusi kabla ajaendelea  kufanya lolote lile alianza kuzungumza.
"mwanangu itabidi uwe mlinzi wa chumba changu,hata panya wadogo wadogo  ufanye juhudi nisiwaone kabisa"

nilimuuliza mama kwa mshangao huku nikifuta machozi kwa kutumia mikono yangu yote miwili.
"mama unamaanisha nini??"
"mwanangu nadya nakufanya dondocha maana umenishida. siku nikihitaji kukurudisha katika ubinadamu wa kawaida nitakurudisha, kwa sasa utakuwa unakaa humu.hamna ambaye ataweza kukuona tofauti na  mimi,pia hautaweza kuongea kitu chochote, mimi tu ndio nina uwezo wa kuongea na wewe"

  Baada ya kuwa mama amemaliza kuniambia hivyo,alitoa ungaunga kwenye kijikopo kile,kisha akanipulizia usoni,
"mama nakufa nakufa,caro nakufa....caro nakufa...baba nakufa...nakufa...."
  Nilitamka maneno yote niliyohisi yatanipa msaada mpaka nikajikuta nabadilika sijitambui,nilishindwa hata kusimama wala kuongea nilichokuwa nakijua ni kuwa mama ni mchawi.cha ajabu panya  alikatisha katika mguu wa mama,nilinyoosha mkono wangu kwa hasira kisha nikamkamata na kuanza kumtafuna.
     Jambo hilo lilimfanya mama aachie kicheko cha dharau
"hahahahahaha,itakubidi mwanangu uzoee hayo ndio maisha,sasa mi natoka kwaheri"

   mama alikuwa anapenda kuongea kwa vitendo hivyo baada ya kumaliza kuongea hivyo alifanya kama alivyosema.

********************
"Hivi huyu mama nadya anafanya ujinga gani huu,anachotakiwa kutambua ni kuwa mimi sijamuozesha na mwanangu aende kumuuwa,hamnaga ndoa ya hivyo ataniulieje mwanangu amemkosea nini???,lazima nilipize kisasi mizimu ya baba na mababu ahsanteni kwa kunipa taarifa hizo  nawashukuru sana mizimu"

***********************
"boss mbona leo nadya ajaja kazini??"
"sijui labda atakuwa anaumwa,mnataarifa yeyote kuhusu yeye??"
"boss,nadya ndio secretary na uchapakazi wake unaujua anawakalibisha wageni kutoka nje ya nchi kuja katika kampuni yetu kwa heshimu ya hali juu itakueje hauna taarifa za mtu kama huyo??"
"jack mpigie nadya ili upate kujua kwa nini hajaja kazini??"
"sawa"

    baada ya muda mchache jack ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya VT ya uchapishaji wa vitabu aliamua kumpigia nadya baada ya muda kadhaa simu ilianza kuita,
"Hallow nandya vipi?"
"nadya hayupo ametoka nje mi mdogo wake naitwa caro"
"mpe simu basi"
"haya"

   Caro aliamka na kumpelekea simu nadya bila ya kujua yaliyomkuta nadya,wakati akiwa ameshatoka nje alikutana na mama yake,
"shikamoo mama?"
"marahaba"
"nadya yuko wapi kuna simu yake inayotoka ofisini"
"lete niongee naye"
"lakini mama nadya yuko wapi ni simu ya muhimu wala haikuhusu wewe kama kuongea nao mi nishaongea nao.

*****************
  Nikiwa chumbani kwa mama niliendelea kusikia majibizano baina ya caro na mama hapo hapo ndipo nilipo kumbuka caro alivyokuwa akinisihi tusali na mimi nikakumbuka kumbe kuna uwezekano mkubwa wa  kumuomba na kumrudia mungu,nilifumba macho huku nikipiga magoti kwa majozi makuu na ya hali ya juu hili mungu awezi kuniokoa katika kifungu kile cha kichawi,
"mungu najua nilikukosea,mungu najua mi nimkosefu muda wote ila wanasema  mungu hamtupi mja wake nadhani hata mimi hivyo hivyo uwezi nitupa,naweka imani yangu yote kwako naomba uniokoe katika adhabu hii katika kifungu hichi cha dhabi,ushetani,uchawi na nguvu za giza,mungu nakutegemea wewe maana wewe ndo msaada wangu katika maisha yangu AMEN"
   Nikiwa nimemaliza maombi ghafla......................
JE NINI KITAENDELEA .......................

LihatTutupKomentar