HANS VAN DER PLUIJM ATOA ONYO SIMBA NA YANGA

KOCHA Mkuu wa Azam FC, Hans van Der Pluijm, amezitaka klabu za Simba na Yanga zijipange kukabiliana na upinzani mkubwa watakapokutana na timu yake kulingana na ubora ilionao kwa sasa.


Mholanzi huyo ameyasema hayo baada ya timu yake ya Azam kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya African Lyon katika Uwanja wa Azam Complex juzi Ijumaa kwenye Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Pluijm alisema anafurahishwa sana na kiwango cha vijana wake ambao wanabadilika kila mechi kulingana na maelekezo anayowapa wakiwa mazoezini.

“Simba na Yanga ni timu za kawaida na wala mimi hazinipi shida kabisa na ukubwa wa majina, ikumbukwe kuwa mchezo wa mpira wa miguu unachezwa uwanjani, hivyo uwezo wa vijana wangu ni mzuri kuliko wale wa Simba na Yanga,” alisema Pluijm.

Azam inaongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 21 ilizojikusanyia mpaka sasa baada ya kucheza mechi tisa.
LihatTutupKomentar