SIMULIZI;UCHAWI WA MAMA.
MTUNZI;RAJA SAIDY.
WHATSAPP;0756920739
SEHEMU YA KUMI NA TISA.
ILIPOISHIA........
police waliweza kumtafuta kila mtaa na kufanikiwa kumpata yule Dereva akiwa katika jalala kuu huku akiwa amechanganyikiwa na kuchafuka mwili mzima,askari hawakujari hilo,waliweza kumchukia dereva yule kisha wakampeleka mahakamani kwa ajili ya hukumu,kutokana na kuwa dereva yule alikuwa amechanganyikiwa hivyo aliweza kusema yeye ndo ameuwa,jaji alitoa hukumu ya kuwa dereva yule afungwe kifungu cha miaka 30 jela,dereva akushangaa kusikia kitu kama hicho kitu alichosema ni kimoja.
"ahsante sana jaji nilikuwa sina sehemu ya kulala hahahahahahaa mungu akubariki"
je nini kitaendele..............
ENDELEA NAYO..........
yalikuwa ni majira ya saa mbili asubuhi mama nadya aliamka huku akionekana kuchoka sana na hii ni kutokana na kuwa alikuwa na msogo wa mawazo juu ya mdogo wake frank aliekuwa anamuumiza kichwa sana na kumfanya ashindwe cha kufanya abaki tu kuwaza na kumuomba mungu haweze kumsaidia ili haweze kumuuwa mdogo wake frank,mama nadya hakukosa wazo kila muda alipofikiria alikuwa akipata wazo jipya,hapo ndipo alipoona kuna maana kubwa ya kuwaita wachawi wenzake,aliweza kushika kibuyu chake kisha akakipuliza na kutamka maneno ya kichawi yaliyofanya kundi kubwa la wachawi kujaa ndani ya kile chumba huku wakiwa pungufu huku wenginne wakiwa na majeraha kadhaa wa kadhaa, kitendo kilichokuwa kinamshangaza mama nadya baada ya kuona mabadiliko makubwa katika kundi lile la wachawi ni baadhi ya wachawi kuja tofauti na muonekano wa kichawi na kuja kawaida kama binadamu wa kawaida.mama nadya akiwa bado anaendelea kufikiria yale mabadiliko ya ghafla, mkuu yule wa wachawi alienusulika kuuwawa na Babu nadya huku akiwa kipindi akiwa chini ya mama nadya alisimama kisha akaanza kuzungumza.
"mkuu utatuwia ladhi pia umetuita kwa ghafla kuja hapa,ila sio vibaya cha muhimu unavyotuona hapa kuna baadhi ya washilika mwenzetu wameshapoteza maisha na hii ni baada ya kuwa umetutuma tumuuwe mkwe wako,sasa basi kuna baadhi ya wachawi hapa kama unavyowaona hawajaja hapa kwa muonekano wa kichawi kuna yule pale na huyu hapa na pia na huyo wa pembeni yako wamekuja kujihudhuru na uchawi pia hata mimi mkuu nimekuja kujihudhuru na uchawi maana nahisi nimetenda dhambi kwa kosa la kumuingilia dereva wa lile Bus la EXPRESS kwa nia ya kukwepa lisasi ya kichawi iliokuwa imepigwa na Babu nadya lakini kutokana na tukio hilo lilinifanya nikae kwenye mwili wa dereva huyo mpaka majira ya usiku,ilipofika majira ya usiku niliweza kumsukuma dereva yule kwa kutumia nguvu za kichawi huku nikiwa bado nipo ndani ya mwili wa huyo dereva, mpaka akaenda kumkata Bibi nadya kitendo kilichofanya apoteze maisha kisha nikatoka ndani ya mwili wa dereva huyo,baada ya kuwa nimetoka nilishuhudia dereva akifanywa na Babu nadya kuwa kichaa,pia hata Babu nadya alijiuwa palepale kwaiyo nahisi nimetenda dhabi nahitaji kumrudia mungu ili apate kunisamehe dhambi zangu"
Baada ya kuwa mchawi yule amemaliza kuongea mchawi mwingine alidakia,
"Mkuu kwa mimi kama mimi siwezi tena kuwa mchawi kwani nimeona hauna faida mkuu,muda tunaotumia kuwalonga wenzetu wenyewe wanazidi kupiga hatua na kufanya maendeleo makubwa kwenye nchi hivyo nimeona pia hata mimi nadhani nchi inanitegeme,mkuu kipindi nilikuwa mdogo nilikuwa na ndoto yakuwa mwalimu wa Sekondary na sikuwa na ndoto ya kuwa mchawi hivyo nahitaji nitimize ndoto yangu"
Baada ya kuwa wachawi wale wameongea mambo mengi yaliyomfanya mama nadya kuinamisha kichwa chini.ghafla Frank aligonga mlango wa Dada yake huku akimuomba afungue na wala hasiwaruhusu wachawi kuondoka,kutokana na kuwa mlango wa mama nadya ulikuwa ujafungwa vizuri na hii ni kutokana na kuwa usiku mama nadya alikuwa na mawazo hivyo hakuweza hata kufunga mlango kutokana na mawazo yaliyokuwa yamemtanda kila sehemu ya mwili hivyo ilimpa nafasi Frank ya kuingia ndani bila ya kukalibishwa na mtu.
***********
Kwakua tulikuwa tuna njaa sana mimi pamoja na mdogo wangu hivyo tuliweza kwenda M-PESA kisha nikatoa hela ili tuweze kupata chakula cha usubuhi katika mgahawa uliokuwa karibu na sisi,nilifanikiwa kutoa kiasi kadhaa kwa ajili ya kupata chakula cha asubuhi,tuliweza kutoka pale M-PESA huku tukiwa tunafuraha kwani hata sisi hatukujua furaha hiyo imetoka wapi,ila kwa upande wetu tuligundua kilichotufanya sisi ni kuwa na furaha ni baada ya kuwa tumefanikiwa kupambana na mchawi kwa kutumia nguvu ya mungu.
Tulipiga sentimita kadhaa kisha tukafanikiwa kuuona mgahawa uliokuwa umeandikwa bango kubwa liliyoonekana vyema.tukiwa tunazidi kupiga hatua ili tuweze kuufikia mgahawa ule,caro aliaanza kusoma maandishi yale kama mtu anaye jifunza kusoma"MAMA JAMES MGAHAWA"
Hatukuchukua muda tulikuwa tayari tumefika katika mgahawa ule,huku moyoni tukijua ya kuwa sisi ndiyo tutakuwa wateja wa kwanza katika mgahawa ule,baada yakuwa tumeingia tulikaribisha na mama aliyoonekana kuwa mtu anayependa ugomvi na hii ni kutokana na kuwa alikuwa na makovu mengi mwilini mwake,aliweza kutuangalia kwa jicho la wizi wizi kisha akatukaribisha kwa sauti iliojaa besi ndani yake.
"Karibuni"
tuliitikia kwa pamoja kisha nikaamuuliza caro.
"caro utakula nini???"
"chochote kile utakacho nichagulia dada yangu"
"sawa"
Nilimuuliza mama yule aliyoonekana kuendelea na shughuli zake za upishi huku akionekana kuwa yuko mwenyewe katika mgahawa ule.
"Mama samahan.kuna nini na nini???"
"kwa sasa mdogo wangu vilivyopo ni chapati,mahalagwe,chai ya maziwa na ya rangi,maana si unajua bado asubuhi kwaiyo bado sijapika vyakula vingine"
"hebu samahani mama nitajie na bei kabisa si unajua sasa hivi tunakula kwa bei"
"Dada kuhusu bei ondoa shaka,chagua unavyovihitaji ntakuambia na bei,pia naomba mkanawe pale kisha mje kukaa"
je nini kitaendelea.................