KOCHA ALLIANCE FC AFUNGUKA KUHUSU KUPANGIWA TIMU

Kocha Mkuu wa Alliance, Mbwana Makata amesema kilichomfanya ashindwe kuwa kwenye benchi la ufundi jana wakati timu yake ikifungwa mabao 5-1 dhidi ya Simba ni kutokana na kuingiliwa maamuzi.

Kabla ya mchezo Alliance walifanya mabadiliko ya mlinda mlango wake kwa kilichodaiwa ni sababu ya kiufundi, walipokea kichapo bila uwepo wa Kocha Mkuu aliyejingo'a kwenye benchi.

"Benchi la ufundi limekuwa likiingilia mipango yangu katika kazi yangu, kikubwa kwenye mechi ya jana tulikuwa tumepanga kikosi cha kuiua Simba, uongozi ukaingilia na kupanga kikosi, nimeamua niwaachie viongozi wafanye kazi," alisema.

Alliance FC wamecheza michezo 11 na kufanikiwa kukusanya pointi 5 wanaburuza mkia kwenye msimamo kwenye ligi Kuu Bara.

LihatTutupKomentar