KOTEI ALITOSA TAIFA LAKE KISA TAIFA STARS


KATIKA kile ambacho kilionekana kuongeza hamasa kwa Watanzania kuelekea katika mchezo wa timu ya taifa hilo, Taifa Stars dhidi ya Uganda ‘The Cranes’, kiungo wa Simba, James Kotei alitangaza kujibadili uraia kwa muda.

Kotei ambaye ni raia wa Ghana, aliamua kutangaza kuwa ataiunga mkono Stars kisha moja kwa moja akasema yeye ni Mtanzania kwa muda na akajipa jina kabisa kuwa anaitwa James Magufuli.

Stars ilikuwa uwanjani juzi kuivaa Uganda katika mchezo wa Kundi L kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon 2019), ushindi pekee ulikuwa na nafasi kubwa ya kuifanya Tanzania ifuzu kucheza michuano hiyo kwa mara ya kwanza tangu ilipofanya hiyo mwaka 1980.

Akitumia ukurasa wake wa Twitter, Kotei aliweka picha kadhaa akiwa amevaa jezi ya Taifa Stars pamoja na baadhi ya mashabiki wengine wa soka ambao nao walikuwa wamevaa jezi hizo.

“Samahani sana Emmanuel Okwi na Juuko Murshid, nimebatizwa upya na jina langu jipya ni JAMES MAGUFULI kutoka Mwanza, Tanzania, nitakuwa nikiiunga mkono Taifa,” aliandika Kotei.

Baada ya hapo akaongeza neno kwa kuandika: “Twendeni Taifa.” Baada ya hapo akaongeza ujumbe mwingine kwa kusema hakuna ambaye amemwandikia maneno ya Kiswahili bali ni yeye mwenyewe ndiye amefanya hivyo
LihatTutupKomentar