KOCHA wa timu ya Singida United, Fred Minziro amesema kuwa kilichoiponza timu yake kupoteza mbele ya Lipuli ni ubutu wa safu yake ya ushambuliaji kushindwa kutumia nafasi walizotengeneza.
Minziro amesema kuwa walicheza kwa umakini ila walishindwa kumalizia nafasi ambazo wamezitengeneza kwenye mchezo wao.
"Ushindani ulikuwa mkubwa na kila mmoja alihitaji matokeo chanya ili asonge mbele ila bahati hakikuwa upande wetu," amesema Minziro.
Michezo ya jana ya kombe la shirikisho ni Lipuli na KMC walitinga hatua ya nusu fainali, huku African Lyon na Singida wakitolewa nje wote kwa kufungwa mabao 2-0