KIGOGO YANGA KUACHIA NGAZI MUDA WOWOTE KUANZIA SASA


Taarifa zilizo chini ya kapeti kutoka ndani ya Yanga zinasema kuwa uwezekano mkubwa vigogo wawili wa klabu hiyo wakaachia ngazi leo, imeelezwa.

Yanga wameitisha kikao na Waandishi wa Habari kitakachofanyika leo majira ya saa sita za mchana huku ikitajwa kuwa viongozi hao watakitumia kuachia ngazi hizo.

Taarifa imeeleza kuwa Kaimu Mwenyekiti Samuel Lukumay pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili pamoja na Mashindano, Hussein Nyika ndiyo waliotajwa kuachia ngazi.

Aidha, Nyika alipogiwa simu kuzungumzia suala hilo alisema ana majukumu mengi ya kikazi na akiomba atafutwe kwa baadaye.

Mbali na Nyika, Lukumay naye alipotafutwa simu yake iliishia kuita mpaka inakata bila kuonesha ushirikiano wowote wa kupokea.

Ikumbukwe klabu hiyo imeshapanga kufanyika kwa mkutano mkuu wa dharura ambao utaamua kama kutakuwa na mkutano mkuu ama wa kujaza nafasi za viongozi walioachia ngazi pekee
LihatTutupKomentar