MANJI AREJEA RASMI YANGA

Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la klabu Yanga Kapteni George Mkuchika amesema Yussuf Manji amerejea katika nafasi yake baada ya kumuandikia burua ya kukubali ombi la Wanachama wa klabu hiyo kumtaka atengue uamuzi wake wa kujiuzulu

Akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya kikao kilichoitishwa na Baraza hilo, Kapteni Mkuchika ameonyesha barua iliyoandikwa na Manji kuridhia kurejea katika nafasi ya Uwenyekiti wa Yanga.

Kapteni Mkuchika amesema Manji aliandika barua ya kujiuzulu lakini wanachama walilikataa ombi lake kupitia Mkutano halali wa klabu hiyo na kumuomba arejee katika nafasi yake.

Barua hiyo aliyoandika ni uthibitisho kuwa ameridhia maombi ya wanachama wa Yanga na sasa ni rasmi amerejea katika nafasi yake.

Kapteni Mkuchika amesema Manji ndio Mwenyekiti wa Yanga huku Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Thobas Langalanga aliyekuwa ameteuliwa kukaimu wadhifa huhatambuliwa

LihatTutupKomentar