AZAM FC WAVUNJA KIBUBU USAJIRI DIRISHA DOGO


Uongozi wa timu ya Azam FC, umesema kuwa baada ya kumsajili mshambulaji Obrey Chirwa bado wapo sokoni kwa ajili ya kuweza kusajili wachezaji wengine kwa ajili ya kuendeleza kuimarisha kikosi chao.

Ofisa habari wa Azam FC, Jaffari Maganga amesema kuwa Chirwa ni mchezaji wa kwanza, bado wanasubiri mapendekezo ya kocha mkuu ili kuweza kujua namna ambayo watafanya kuboresha zaidi kikosi.

"Tumeanza na Chirwa huo ni mwanzo tu kwetu, tunajua kwamba kuna ushindani mkubwa kwenye ligi, malengo yetu ni kuweza kushinda tunatakiwa kujiimarisha zaidi.

"Tumefanikiwa kuwa nafasi ya kwanza mpaka sasa bila kupoteza mchezo hata, tunahitaji kuongoza zaidi na kuwa na mipango madhubuti ambayo itatufanya tuendelee kubaki kileleni," alisema.

Azam wamecheza michezo 12 kwenye ligi kuu, wametoa sare michezo 3 na kushinda michezo 9 na kujikusanyia pointi 30 wakiwa ni vinara wa ligi.

LihatTutupKomentar