SIMULIZI;UCHAWI WA MAMA. MTUNZI;RAJA SAIDY. WHATSAPP;0756920739

SIMULIZI;UCHAWI WA MAMA.
MTUNZI;RAJA SAIDY.
WHATSAPP;0756920739.

SEHEMU YA SABA.

ILIPOISHIA.........
"basi sawa we sio mtoto ila ukirudi kijijini ndio utampata mke wako huko maana tumeshaanza kuwarudisha pole pole"
kutokana na kauli ile ya mkuu wa wachawi ilimfanya babu nadya kugeuka nyuma kwa lengo la kumuangalia mke wake kama yupo,alianza kupatwa na hasira pindi tu alipongudua mke wake hayupo ,wale wachawi wengine  wamesha mchukuwa,kutokana na kitendo kile babu nadya alikasirika kwa kuingiza mkono wake mfukoni kisha akabadilika na kuwa fisi
"jambo lile lilimshangaza mkuu wa wachawi na kuanza vita mpya kabisa na babu nadya mzee mwenye nguvu za mizimu........
je nini kitaendelea...................

ENDELEA NAYO..............

*************
Niliweza kufanya maamuzi kutoka kwenye akili yangu,baada ya kuona muda unazidi kukatika bila ya kufikiria kitu chochote,machozi ya uchungu yaliendelea kunitoka na kunifanya wakati nikitaka kusaini najikuta natetemeka sana.jambo ili lilipelekea muda uzidi kwenda na kunifanya mimi nichukue maamuzi magumu ya ujasiri ili niokoe thamani ya mdogo wangu.  bora aendelee kuishi huku akiwa mlemavu kuliko kupoteza vyote nakuweza kukumbwa na umauti,nilifanya maamuzi ya dakika moja kisha nikachukua karatasi kwa lengo la kusaini huku nikiwa mwenyewe katika kile chumba cha daktari.sikuwa na hofu kuhusu ni namna gani taarifa itamfikia daktari maana tayari alikwisha niambia baada ya nusu saa atakuja kuchukua majibu.
    Niliivuta katarasi na kushikilia biki kwa ujasiri huku machozi yakiendelea kunitoka na kuidondokea ile karatasi,jambo hilo lilinifanya niumie lakini nilikuwa sina jinsi kwa wakati huo,nilianza kushika biki kwa nguvu zangu zote kisha nikatazama mahali palipo andikwa "SIGN...................."nikajikaza kisha nikaanza kusaini katika ile deshi iliyombele ya neno SIGN,cha ajabu kila nilivyojaribu kusaini nilikuwa nahisi mwili unakuwa mzito,ghafla alikuja nyuki niliyoshindwa kujua ametokea wapi!!!!! kisha akaning'ata kwenye kidole kilichokuwa kimeshikilia biki,ghafla mkono wangu ulianza kuuma kitendo kilichonifanya nipige yowe kali za maumivu zilizochanganyana na mkwaluzano wa sauti,kitendo kile kilinifanya niwe katika hali ya uchizi na kushangaa wapi  nyuki anaweza kumuuma binadamu bila sababu ya msingi.wakati nikiendelea kukumbuka hivyo basi nazidi kupiga yowe kali maana niligundua huo utakuwa uchawi wa mama na sio kitu kingine.
       nilipelekwa  kwenye chumba kilichoandikwa ACU chumba cha wagonjwa mahututi kisha nikaanza kufanyiwa uparesheni ya mkono wa lengo la kutoa kile kilicho ndani ya kidole changu  kinachonifanya niumie.cha ajabu kabla hata madaktari hawajaanza kunifanyia uparesheni tayari nilikuwa nimesharudi katika hali yangu,kitendo hicho kiliwashangaza hata madaktari waliokuwa wamepangwa kunifanya oparesheni maana nilisikia wanasema tangia wazaliwe hawajawahi kuona kitu kama hicho.baada ya kuwa nimesharuhusiwa niliweza kukaa katika bechi za kusubili wagonjwa niliangalia mudaa katika saa yangu ya mkononi,tayari ilikuwa imetimia saa 10:30 jion ,maana hata tayari muda wa kusaini umeisha,kitendo kilichofanya nianze kushikwa na mawazo juu ya mdogo wangu kwa kushindwa kusaini kwani nimehatarisha maisha yake.
  kama kawaida yake yule nesi mnene akaja kuniita kwa ishara kwani hata yeye tayari alikuwa ameshaanza kuniongopa kutokana na tukio la ghafla lililokuwa limenitokea,niliweza kumfuata kwa nyuma nyuma mpaka pale alipo nionyesha kwa ishara mahali napo takiwa kuingia,nilifanya kama alivyo nielekeza.
nilishindwa kuamini  macho yangu baada ya kumkuta mdogo wangu akiwa mzima tena wa afya,kisha akaniita huku akidondosha machozi
"Dada nadya Dada nadya"
niliweza kupiga hatua chache mpaka pale alipo kisha tukakumbatiana,
"mdogo wangu caro unaendeleaje???"
"Dada mimi ni mzima hata nashangaa mguu umepona ghafla tu hapa nasubili ruhusa kutoka kwa madaktari"
"pole sana mdogo wangu"
"ahsante dada nadya"
    Tukiwa tunaendelea na mazungumzo yetu tulisikia sauti ya mtu ikizungumza huku ikwa inajirudia rudia (mwangwi) iliyotufanya tukumbatiane kutokana na uoga tuliyokuwa nao.
"wanangu wanangu mimi  baba yenu baba yenu,nipo karibu yenu chochote mnachoona kinaendelea ni msaada kutoka kwangu,wanangu mnapoenda nyumbani kueni  na  tahadhari kwa mama yenu kwani ni mtu mbaya sana,aliweza kuniuwa kisha akala nyama yangu akiwa na wachawi wenzake,mwanangu nadya mimi ndiye niliwafanya mbishane na mdogo wako ili msilale kitandani kwani mama yako alikuwa amewategea dawa kwa ajili ya kuwauwa,pili wewe caro ulikuwa aumwi yalikuwa ni mauzauza ambayo yangefanya ukatwe mguu hivyo nikaamua kutuma nyuki ili aweze kumng'ata nadya ili ashindwe kusaini,sasa basi nawaombeni kueni makini mimi nipo jirani nyuma yenu popote mlipo,ila mfanye juu na chini mama yenu asingundue kama nawasaidia maana anao uwezo wa kunirudisha nilipotoka safari njema"

***********
    mama nadya aliweza kusimama na kupata nafuu baada ya muda mfupi toka apoteze fahamu,kutokana na kitendo kile cha kupigwa kofi la kichawi na nadya kilimkera na akagundua hapa itakuwa anapambana na nguvu ya ziada inayomsaidia nadya na caro hivyo akaamua kuwaita wachawi wenzake kwa ajili ya kulizungumzia jambo hilo,mama nadya bila kupoteza muda aliingia chumbani mwake kisha akainama chini ya kitanda na kuchukua kibuyu kisha akaenda nacho sebuleni.
     mama nadya alianza kupuliza kibuyu kile huku akiendelea kutamka maneno aliyoyajua yeye mwenyewe,baada ya muda mchache walitua pale kundi kubwa la wachawi  kisha wakaanza kucheza ngoma za asili kabla hata ya kuanza kuzungumza.wakiwa tayari wameshamaliza kila kilichotakiwa kufanywa kabla hawajaanza mazungumzo,mama nadya alianza kwa kusema,
"nimewaiteni hapa kwa msaada mmoja.nyie mnajua mimi sishindwi na kitu"
"Ndio,ndio mkuu"
"kwa sasa nahisi kuna mtu anatumia nguvu za ziada kuwasaidia wakina nadya na caro sina huakika kama ni mungu au laah ila najua ni mzimu ila mpaka sasa sijui ni mzimu upi ila nahitaji msaaada wenu"
mchawi mmoja alisimama kwa niaba ya wengine huku wote wakiwa wako uchi wa mnyama,
"nachokushauli mkuu mi nina dawa nimeitoa zimbabwe huko ndo inapatikana tu kazi yake ni kuzuia mizimu sa cha msingi we ichukue iweke kwenye maji kisha uanze kumwaga hayo maji yake kwa kila mlango wa humu ndani.kazi hii ifanye kabla hata wanao hawajarudi,baada ya hapo kama walikuwa na mzimu utashindwa kuingia ndani utakuwa unaishia nje hivyo utakifanya kila unachokitaka"
"ahsante sana mshilika ndo maana nawategemea,si mnajua mi sina muda maalumu wa kazi ngoja nianze kuiweka hii dawa ili ianze kufanya kazi kabla hawajaja
je nini kitaendelea................

LihatTutupKomentar