AZAM FC WATOA KIPIGO KWA KAGERA SUGER

AZAM FC imendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuwachapa wenyeji, Kagera Sugar 1-0 mchana wa leo Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Ushindi huo umetokana na bao pekee la mshambuliaji Mzimbabwe, Donald Dombo Ngoma aliye katika msimu wake wa kwanza tangu asajiliwe kutoka Yanga SC aliyefunga dakika ya 40, kabla ya kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 90 na ushei.
Na sasa timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake inafikisha pointi 30 baada ya kucheza mechi 12, ikiendelea kuongoza Ligi Kuu.

LihatTutupKomentar