OKWI AFUNGUKA HAYA BAADA YA USHINDI WA JANA



Baada ya kufikisha mabao 4 kwenye ligi kuu mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi amesema kuwa mambo makubwa yanakuja.

Okwi ambaye msimu uliopita alifunga mabao 20 leo ameiongoza Simba kupata ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Alliance, amefunga mabao 2 hali iliyofanya waweze kuchukua point 3 muhimu .

"Nitajihidi kupambana kwa ajili ya timu yangu na kufunga,sina mawazo ya kuwania ufungaji bora kwa sasa hilo ni jambo la kusubiri hadi mwisho wa ligi, ninafurahia kufunga naweza kusema kuwa kazi imeanza mashabiki waendelee kutuunga mkono," alisema.

Ushindi huo wa Simba unaifanya kuwa timu ya kwanza kufunga mabao zaidi ya manne ndani ya ligi, yanaifanya kufikisha pointi 20 baada ya kucheza michezo 9 na kushika nafasi ya pili wakiwa nyuma ya Azam yenye point 24 ikiwa imecheza michezo 10.

LihatTutupKomentar