FC BARCELONA YASHINDA BILA MESSI YAANZA MAISHA MAPYA

Club ya FC Barcelona ya Hispania usiku wa October 24 2018 ilianza maisha rasmi bila ya uwepo staa wao Lionel Messi ambaye kwa sasa anauguza jeraha lake la mkono wa kulia litakalomuweka nje ya uwanja kwa wiki tatu.
Messi akiwa jukwaani leo ameishuhudia club yake ikicheza game yake ya tatu ya UEFA Champions League hatua ya makundi dhidi ya Inter Milan ya Italia, pamoja na Barcelona kumkosa Messi mchezo ulimalizika kwa FC Barcelona kushinda kwa magoli 2-0.
Magoli ya Barcelona yamefungwa na Rafinha dakika ya 32 na Jordi Alba dakika ya 83, ushindi huo unawafanya Barcelona waongoze kundi B kwa kufikisha jumla ya point tisa wakifuatiwa na Inter Milan wenye point sita, Tottenham na PSV wapo nafasi ya tatu kwa kuwa na point moja

LihatTutupKomentar