YANGA WAMEKIAMSHA HUKO MORO TIZI LAKE NI BALAAA



Homa ya watani wa jadi ikiwa inaendelea unaambiwa kikosi cha Yanga kimezidi kujifua huko Morogoro tayari kuchuana na Simba Jumapili ya wiki hii.

Kocha Mkuu Mwinyi Zahera ameanza na mazoezi ya kuwapa pumzi wachezaji wake ili kuhakikisha wanamudu dakika zote 90 bila kuchoka ili kuwahimili Simba.

Zahera ameanza na programu hiyo kutokana na kikosi cha wachezaji wake kuonekana kuchoka kila ifikapo dakika za mwisho kuelekea mwishoni mwa mchezo.

Yanga imepiga kambi mjini Morogoro kwa siku 5 kabla ya kurejea Ijumaa au Jumamosi ya wiki hii Dar es Salaam tayari kumalizana na Simba.

Timu hizo mbili zitakuwa zinakutana kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam Jumapili ya Septemba 30 2018.

LihatTutupKomentar