DISMAS TEN AMETABIRI MECHI YA SIMBA VS YANGA LEO

Wakati wadau na mashabiki wa mpira wa miguu nchini wakisubiria kwa hamu kipute cha mechi ya watani wa jadi katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, unaambiwa Ofisa Habari wa Yanga, ametabiri Simba kufa 4-1.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Dismas Ten ametabiri kuwa Simba itafungwa jumla ya mabao 4-1 na Yanga katika mchezo ambao utaanza majira ya saa 11 jioni.

Ten aliweka picha inayoonesha 1-4 ambapo 1 ikiwa na rangi nyekundu huku 4 ikiwa na rangi ya njano ikimaanisha kuwa Yanga itashinda mabao 4-1.



Yanga itaingia uwanjani ikiwa haina presha yoyote kufuatia kutopoteza mchezo hata mmoja huku Simba wakienda sare mmoja na kufungwa katika mechi 4 walizopiga msimu huu.

Mechi hiyo yenye msisimko wa aina yake tayari imeteka vinywa vya mashabiki kwa wiki hii nzima ambapo leo jioni itajulikana mbivu na mbichi kwa watani hao wa jadi.

LihatTutupKomentar