Kizuri chajiuza. Ni msemo wa wahenga ambao utakuwa unamhusu kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Ubelgiji THIERRY HENRY. Mkongwe huyo wa zamani ambaye aliwahi kucheza katika klabu ya Arsenal kwa mafanikio makubwa kabla ya kutimkia katika klabu ya Barcelona. Taarifa zinadai kuwa klabu ya Aston Villa inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Uingereza imeanza mazungumzo na mkogwe huyo wa soka ili aje achukua mikoba ya kocha Steve Bruce ambaye ameonekana kutokufanya vizuri katika klabu hiyo. Henry ameushawishi uongozi wa Aston Villa kumsajili kocha huyo baada ya kufanya vizuri akiwa na timu ya taifa ya
Ubelgiji ambapo timu hiyo mwaka huu imefanikiwa kufika hatua ya nusu fainali katika michuano ya kombe la dunia iliyofanyika nchini Urusi kabla ya kuondolewa na timu ya taifa ya Ufaransa.
Ubelgiji ambapo timu hiyo mwaka huu imefanikiwa kufika hatua ya nusu fainali katika michuano ya kombe la dunia iliyofanyika nchini Urusi kabla ya kuondolewa na timu ya taifa ya Ufaransa.