CHIRWA NAE APELEKWA TFF

Uongozi wa klabu ya Mbeya City umetuma barua katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ukilalamikia maamuzi ya Mwamuzi aliyechezesha mchezo wao dhidi ya Yanga kuwa hakuumudu.
Mbeya City wameeleza mapungufu kadhaa ambayo Mwamuzi alishindwa kuyahimili wakati wa mechi hiyo ya ligi kuu iliyopigwa Aprili 22 2018 kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Barua hiyo imeeleza tukio la Juma Mahadhi kufanyiwa faulo ambayo ilizaa bao la kwanza kwa Yanga ikisema kuwa si halali.
Vilevile imeelezea tukio la mchezaji Mshambuliaji wa Yanga, Mzambia, Obrey Chirwa kumtwanga kiwiko mchezaji wa Mbeya City katika mchezo huo.
Tayari uongozi huo umeshawasilisha barua hiyo kunako makao makuu ya TFF yaliyo mitaa ya Karume, Ilala, jijini Dar es Salaam.

LihatTutupKomentar