USIKU WA UEFA BAYERN VS MADRID

Nusu fainali ya UEFA Champions League kuendelea leo kwa mchezo mmoja unaozikutanisha timu za Real Madrid na Bayern Munich mara baada ya kuzishuhudia klabu za Liverpool na AS Roma hapo jana.
Katika historia ya michuano hii, hakuna mchezo ambao umekutanisha timu mbili mara nyingi katika mchezo huu wa leo. Kiujumla wanaume hawa wameshakutana mara 24 katika hatua tofauti za Champions League, mara ya mwisho ni msimu uliopita katika robo fainali ambapo Madrid alishinda mechi zote mbili na kwenda mpaka fainali kubeba taji la pili mfululizo.
Mchezo wa leo utakuwa wa 25, Kila timu imeshinda mechi 11 na sare 2. Hivyo leo anatafutwa mbabe wa jumla.
Leo pia itakuwa mara ya 7 timu hizi zinakutana katika hatua ya nusu fainali ya michuano hii - Madrid akiwa na rekodi ya kumfunga Bayern katika mechi 5 zilizopita za UCL, akifunga magoli 13 na kuruhusu manne 4 tu.
Madrid leo anaweka rekodi ya kucheza hatua ya nusu fainali ya mara 8 mfululizo, wakati Bayern ikiwa wanacheza nusu fainali ya 6 katika kipindi cha miaka 7 iliyopita.

LihatTutupKomentar