HABARI, TETESI NA MATUKIO ULAYA

HABARI, TETESI NA MATUKIO ULAYA
Na Godfrey Mgaya 
 Jumanne 1 May 2018
Arsenal wameimarisha ofa yao kwa kiungo wa kati Jack Wilshere. Mkataba wa mchezaji huyo wa miaka 26 unafikia kikomo mwisho wa msimu na amekuwa akitafutwa na Wolves na Everton. (Mirror)

Mchezaji anayesakwa sana na Liverpool Max Meyer hatachezea tena Schalke baada yake kufukuzwa kutoka mazoezini na kutoka kwenye kikosi cha kwanza. Meyer, mshambuliaji mwenye miaka 22, aliadhibiwa baada yake kumkosoa mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo ya Bundesliga Christian Heidel. (Sky Sports)

Rais wa Real Madrid Florentino Perez amesema Gareth Bale, 28, anataka kusalia Bernabeu licha ya tetesi kwamba huenda mshambuliaji huyo wa Wales akahama. (Sun)

Pep Guardiola amesema uamuzi ufaao utafanywa kuhusu kipa wa Manchester City Joe Hart iwapo West Ham wataamua kutobadilisha mkataba wake wa sasa wa mkopo kuwa uhamisho wa kudumu. (Mirror)
Marouane Fellaini, 30, anataka Manchester United wampe mkataba wa muda mrefu zaidi kushinda mwaka mmoja ambao wamemuahidi kwa sasa Old Trafford. (ESPN)

Kiungo wa kati wa Arsenal Santi Cazorla anatumai kwamba ataweza kurejea kucheza kabla ya mwisho wa msimu. Mhispania huyo mwenye miaka 33 hajachezea Gunners tangu mwaka 2016 kutokana na jeraha la mguuni ambalo limekosa kupona. (AS)

Meneja wa Shakhtar Donetsk Paulo Fonseca amekataa ofas kutoka kwa Everton baada ya kuanza kuangazia kumrithi Arsene Wenger Arsenal, kwa mujibu wa mwanahabari Guillem Balague. (Express)

Thierry Henry na Tony Adams ni miongoni mwa watu mashuhuri 100 wa Arsenal ambao wamealikwa kwa mechi ya mwisho ya Wenger nyumbani, ambapo watasherehekea miaka 22 ya Mfaransa huyo katika klabu hiyo. (Mail)

Mshambuliaji wa West Ham Andy Carroll, 29, alifukuzwa kutoka mazoezini Jumatatu na meneja wa klabu hiyo David Moyes baada ya wawili hao kukorofishana. Klabu hiyo inatarajiwa kuanza uchunguzi kuhusu kisa hicho. (Telegraph)

Wolves ambao wamepanda daraja kucheza Ligi ya Premia watakuwa wanamtaka kipa wa Stoke Jack Butland iwapo klabu yake itashushwa daraja. Mchezaji huyo wa kimataifa wa England wa miaka 25 pia anatafutwa na Liverpool na West Ham. (Express)
Beki wa Manchester United Ashley Young amesema atasikitika sana kuhusu msimu huu hata kama watafanikiwa kushinda Kombe la FA. (ESPN)
Meneja wa Bournemouth Eddie Howe amevunjwa moyo na uchezaji wa klabu hiyo karibuni, huku wakiwa wamecheza mechi tano sasa bila ushindi. (Bournemouth Daily Echo)
Sunderland wanamtaka straika wa zamani Kevin Phillips, 44, awe meneja wao baada ya kuondoka kwa Chris Coleman kufuatia kushushwa daraja kwa klabu hiyo hadi League One. Phillips, aliyefunga mabao 116 katika mechi 210 ligini akichezea klabu hiyo kwa sasa ni mkufunzi Derby. (Sun)
Meneja wa Everton Ronald Koeman amesema amesikitishwa na mchezaji Davy Klaassen waliyemnunua mwanzo wa msimu. Nahodha huyo wa zamani wa Ajax ameshindwa kuvuma katika soka England. Mholanzi huyo Klaassen, 25, amewachezea mechi 14 pekee msimu huu. (Liverpool Echo)
Winga wa Watford Gerard Deulofeu, kwenye Twitter, alishangazwa na hatua ya kuachwa kwa jina lake kwenye jezi ya Barcelona ya kusherehekea kushinda ligi. Mhispania huyo wa miaka 24 yupo Watford kwa mkopo lakini alichezea Barca mechi 10 kabla ya kuhamia England. (Mail)

Kipa wa Penarol Kevin Dawson alilazimika kuomba jezi kutoka kwa shabiki baada yake kusahau jezi yake nyumbani kabla ya klabu yake kucheza dhidi ya Progreso katika ligi kuu ya Uruguay, Primera Division. (Mail)
LihatTutupKomentar