YANGA VS SIMBA YAJUE HAYA

Zikiwa zimesalia siku tano pekee kueleka mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza kuimarisha zaidi ulinzi.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo, amesema kuwa jumla ya Camera 109 zitafungwa Uwanjani kuelekea mechi hiyo inayoteka hisia za mashabiki na wadau wa soka nchini.
Clifford ameeleza kuwa Camera hizo zitafungwa ili kuimarisha ulinzi na usalama ndani ya Uwanja ambapo zitakuwa zinarekodi matukio mbalimbali kabla na baada ya mchezo.
Mechi hiyo inatarajiwa kupigwa Aprili 29 2018 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Tiketi za mchezo huo zimeshaanza kuuzwa kupitia Selcom na kwale wote ambao hawajanunua wanaweza kuzipata muda wowote.

2 : Beki wa klabu ya Simba, Salum Mbonde, amesema kuwa wanaendelea kujipanga kuelekea mechi dhidi ya watani wao wa jadi Yanga itakayopigwa Uwanja wa Taifa.
Beki huyo ambaye amekosa mechi nyingi msimu huu kutokana na kuwa majeruhi, amesema mechi hiyo itakuwa si nyepesi wala ngumu, kwani atakayejipanga atapata matokeo.
Mbonde ameeleza kuwa mechi inayokutanisha timu hizo za Kariakoo inakuwa ni ya aina yake na si rahisi kutabirikakama wengi wanavyozania.

Simba na Yanga zote zipo Morogoro hivi sasa kujiandaa na mechi hiyo.

LihatTutupKomentar