CHELSEA YAMSAJIRI GOLIKIPA

Na MOSES FRANCIS
Wakati ligi kuu ya Uingereza ikikaribia kuanza kupamba moto timu mbalimbali zinazoshiriki ligi hiyo kubwa duniani zimeendelea kuimarisha vikosi vyao kwa kusajili wachezaji mbalimbali. Unaambiwa hivi katika klabu ya Chelsea kocha wao mpya Maurizio Sarri hana masihara kabisa. Siku ya leo kocha huyo amekamilisha usajili wa golikipa ROBERT GREEN kutoka katika klabu ya Hundersfield. Golikipa huyo mwenye umri wa miaka 38 amekuwa na kiwango kizuri ndani ya klabu ya Hundersfield msimu uliopita mpaka kufikia mabosi wa klabu ya Chelsea kumvuta golikipa huyo mgongwe na kumleta darajani. Hali hii huenda ina ashiriainaashiria kuwa huenda golikipa namba moja wa klabu hiyo Thibaut Courtois akaondoka ndani ya klabu hiyo siku chache zijazo licha ya kuwa amesaini mkataba wa mwaka mmoja ndani ya klabu hiyo ya jijini London.

LihatTutupKomentar