POGBA ANARUDI JUVENTUS.

Na MOSES FRANCIS 
Hao Juventus moto wao ni hatari usiguse. Inshu iko hivi kwa sasa wamefanikiwa kumsajili mshambuliaji Cristian Ronaldo kutoka katika klabu ya Real Madrid kwa thamani ya paund milion 99. Ili kuimarisha zaidi  kikosi chao kinachonolewa na kocha Maxmilian Allegri timu hiyo ina mpango wa kumuuza kiungo wao raia wa Bosnia Miralem Pjanic ili waongezee pesa za kumsajili kiungo wao wa zamani aliyetimkia katika klabu ya Manchester United Paulo Pogba. Lazima ikumbukwe kuwa Pogba amekuwa akionyesha kiwango kikubwa sana pala anapokuwa anaichezea timu yake ya Ufaransa ambayo imeibuka bingwa wa kombe la dunia mwaka huu
Klabu ya Juventus ina matumaini ya kumsajili kiungo huyo wa Manchester United ili aje acheze pamoja na mshambuliaji Cristian Ronaldo ambaye walimsajili kutoka katika klabu ya Real Madrid.
LihatTutupKomentar