Mawakili wa Arsenal wamekuwa wakiwasiliana na klabu ya Manchester City kuhusu Mikel Arteta kuwa mkufunzi mpya wa Arsenal.
Raia huyo wa Uhispania bado yupo chini ya kandarasi ya City huku klabu hiyo ikisubiri Arsenal kuilipa fidia.
Mkutano wa kaimu mkufunzi Freddie Ljungberg ulifutiliwa mbali siku ya Alhamisi.City imekasirishwa na jinsi Arsenal ilivyochukulia swala hilo tangu siku ya Jumapili.
The Gunners walishindwa kusema kwamna wana hamu ya kumsajili raia huyo mwenye umri wa miaka 37 ili kuchukua mahala pake Unai Emery licha ya timu hizo mbili kukutana katika uwanja wa Emirates , lakini baadaye wakawatuma maafisa wake wao wawili kwa mkutnao wa usiku na Arteta kufuatia ushindi wa City wa 3-0 dhidi ya Arsenal katika uwanja wa Emirates.
Hatahivyo hakujakuwepo na mawasiliano yoyote ya maafisa wa kuu wa Arsenal kwa City , ambao hawamlaumu Arteta ambaye amekuwa akimpasha mkufunzi Pep Guardiola kila yanayojiri.