TETESI ZA USAJIRI BARANI ULAYA


Everton wanataka kumuajiri aliyekuwa mkufunzi wa Watford Marco Silva ili kuchukua mahala pake Sam Allardyce. (Goal)

Bayern Munich itawasilisha ombi la kutaka kumsajili mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala, 24, iwapo watampoteza mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski, 29, mwisho wa msimu huu. (Bild, via Sun)

Arsenal imeibwaga Bayern Munich katika usajili wa beki kinda wa Uturuki mwenye umri wa miaka 21 Caglar Soyuncu, ambaye anaichezea klabu ya Freiburg nchini Ujerumani Bundesliga . (Evening Standard)

Crystal Palace inatarajiwa kufanya mazungumzo ya kandarasi mpya na kiungo wa kati wa Ufaransa Yohan Cabaye, 32, na beki wa Uingereza Joel Ward, 28, wiki ijayo ili kuweka wazi hatma yao katika klabu hiyo.. (Guardian)

Aston Villa itajaribu kumnunua kiungo wa kati wa West Brom Gareth Barry, 37, katika klabu hiyo iwapo watapandishwa daraja kutoka ligi ya mabingwa nchini Uingereza hadi ile ya premia. (Mirror)

Everton, Leicester na Burnley wote wana hamu ya mshambuliaji wa Misri mwenye umri wa miaka 23 Mahmoud Hassan, ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Uturuki ya Kasimpasa kutoka klabu ya Anderlecht. (ESPN)

Kiungo wa kati wa Manchester United Marouane Fellaini na wawakilishi wake wataendelea na mazungumzo na Manchester United kuhusu mkataba mpya. Kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 inakamilika mwisho wa msimu huu. . (Sky Sports)

Mkufunzi wa Stoke Paul Lambert amepinga ripoti zinazowahusisha mabingwa wa ligi ya mabingwa nchini Uingereza Wolves na ununuzi wa kipa wa Uingereza Jack Butland, 25 kwa dau la £35m. (Express and Star)

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp anataka kumnunua winga wa Borussia Dortmund na Marekani Christian Pulisic, 19, huku pia Arsenal ikimnyatia. (Mirror)

West Brom inataka kuwasilisha maombi ya kusajili mmoja ya makocha watatu .Watatu hao ni mkufunzi wa Bristol City, Lee Johnson, kocha wa Brentford Dean Smith na naibu kocha wa Leicester Michael Appleton. (Sky Sports)

Mkufunzi wa zamani wa Leicester City Claudio Ranieri ameitishia Nantes kumfuta kazi baada ya rais wa klabu hiyo kumshutumu kwa kukosa utaalam. (Leicester Mercury)

Kipa wa Ubelgiji Simon Mignolet, 30, anasema kuwa atasubiri hadi mwisho wa msimu wa kombe la dunia kabla ya kuamua iwapo ataondoka Liverpool. (ESPN)

LihatTutupKomentar