Aliyekuwa Mjumbe wa Baraza la Wadhamini wa klabu ya Simba, Mzee Hamis Kilomoni, ameibuka na kudai kuwa Simba haijafuata katiba baada ya kuitisha Mkutano Mkuu wa dharura utakaofanyika Mei 20 2018.
Kilimoni ameeleza kuwa Simba imeenda kinyume na katiba kitu ambacho anakipinga huku akisema wanachama wake wamekuwa wakivutwa bila kujijua.
Mzee huyo ambaye ameonekana kupinga mchakato wa mabadiliko kwa muda mrefu, amezungumza hayo akipinga Simba kuitisha mkutano huo.
Simba imetangaza kuitisha mkutano huo kwa ajili ya mabadiliko ya kikatiba huku ikielezwa ndiyo itakuwa safari ya mwisho ya kumkabidhi rasmi mzabuni wake, Mohammed Dewji Mo.
Mkutano huo utafanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano uliopo mitaa ya Ocean Road jijini Dar es Salaam.