MANARA AZIDI KUTAMBA JINSI MCHAKATO UNAVYO KWENDA

Wakati klabu ya Simba ikitangaza kuwa na mkutano mkuu, Ofisa Habari wa Simba ametumia nafasi yake kutamba dhidi ya wapinzani wao.

Akitumia ukurasa wake wa Instagram, kama kawaida yake, Manara ametambia mkutani huo ujao huku akidai wanaenda kumalizia kazi ya mchakato wa uwekezaji huku akimtupia dongo ofis habari wa Yanga, Dismas Tena ambaye alihusika kuandaa jarida la klabu yake hivi karibuni.

Manara ameandika haya: “Tunakwenda kukamilisha mchakato rasmi tarehe 20 mwezi huu..Mpira ni pesa sio porojo za kutegemea kuuza majarida..na uzuri wake MO anakuja kuwekeza pesa..ni pesa tu.....tunahesabu siku tubadilishwe hadhi...ila tunaomba kombe letu mapema kwa hiyari yenu....hahahahaha naambiwa foreigners kaenda mmoja tu..wengine hadi wapewe mishahara

“Acha nicheke kigongowazi😁😁🏌🏽♀😁😁🏌🏽♀ #ThisIsSimba #SimbaScNguvuMoja 🇮🇩🇲🇨🙏”

LihatTutupKomentar