Sikia haya kutoka Chelsea

Nahodha msaidizi wa klabu ya Chelsea, Cesar Azpiliqueta amepewa adhabu ya kukatwa mshahara wa wiki moja na uongozi wa klabu ya Chelsea kwa kosa la wizi. Azpiliqueta alikutwa na kitabu cha notes ambacho ni mali ya kiungo wa klabu hiyo, Cesc Fabregas. Siku ya Jumatatu, Fabregas alipeleka mashtaka kwa uongozi wa klabu baada ya kutafuta kitabu chake chenye notes za kupiga pasi za magoli bila mafanikio hali ambayo ilifanya uongozi kupitisha msako mkali kwenye chumba cha kila mchezaji. Baada ya msako huo, kitabu hicho ambacho ni mali ya Fabregas kilikutwa kwenye kabati la Cesar hivyo kupelekea adhabu hiyo. Azpiliqueta ameshatoa assist nne za magoli mpaka sasa ambapo magoli yote hayo yakifungwa na Morata.
LihatTutupKomentar