Mechi ya Barcelona yachezwa bila Washabiki Uwanjani washinda 3-0

Vurugu za maandamano zilizotokea nje ya Uwanja wa Camp Noun a katika mitaa kadhaa ya Jiji la Barcelona imesababisha mchezo kati ya Barcelona dhidi ya Las Palmas kuchezwa bila mashabiki.
Vurugu hizo zilitokana na maandamano ya kiasiasa ambapo kumekuwa na presha kubwa juu ya Jimbo la Catalunya ambapo ndipo ilipo Barcelona kutaka ijitenge na iwe taifa huru kutoka ndani ya Hispania.
Polisi walitumia nguvu kubwa kuzuia maandamano hayo lakini hali ilikuwa ngumu na ilibaki kidogo mchezo huo wa La Liga usiishwe kuchezwa.
Lakini baada ya kushauriana kwa dakika kadhaaa  ndipo mchezo huo ukachezwa bila mashabiki kuruhusiwa kuingia uwanjani.
Pamoja na hivyo, Barcelona imepata ushindi wa mabao 3-0 wafungaji wakiwa ni Sergio Busquets aliyefunga katika dakika ya 49 pamoja na Lionel Messi aliyefunga mabao mawili dakika ya 7
0 na 77
LihatTutupKomentar