TOWSHIP ROLLES WAANZA KUOGOPA YANGA KUELEKEA MECHI YAO YA LEO



THOMAS Trucha, Kocha Mkuu wa Township Rollers amesema kuwa wapo tayari kwa ushindani wa leo mbele ya Yanga kwenye mchezo wa kimataifa dhidi ya Yanga. 

Rollers leo itamenyana na Yanga uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa awali kabla ya ule wa marejeano utakaochezwa Botswana kati ya Agosti 23-25. 

"Ntegemea mchezo utakuwa mgumu na wenye ushindani, tumejipanga kufanya vizuri na kupata matokeo chanya kwenye mchezo wetu wa leo. 

"Mchezo hautakuwa mwepesi ila tupo tayari mashabiki watupe sapoti," amesema. 

Timu hizo zilipokutana mwaka 2018 Yanga ilipoteza nyumbani kwa mabao 2-1 kabla ya kwenda kutoka sare Botswana.

LihatTutupKomentar