ALLIANCE FC WAVITAMBIA VIGOGO TPL


UONGOZI wa Alliance FC 0 kuwa msimu ujao utawafundisha soka la darasani vigogo wa ligi ikiwa ni pamoja na Yanga, Simba pamoja na Azam FC.

Alliance ambayo msimu ujao utakuwa ni msimu wake wa pili kwa sasa ipo chini ya Kocha Mkuu, Athuman Bilal aliyekuwa akiinoa Stand United na amesaini kandarasi ya miaka miwili.

Akizungumza , Ofisa Habari wa Alliance, Jackson Mwafulango amesema kuwa msimu mpya watakuwa tofauti zaidi ya msimu uliopita.

“Msimu uliopita tulikuwa na sera ya kusambaza misumari ya upendo, safari hii tumejipanga kabisa kuwapa mpira wa darasani wapinzani wetu na kupata matokeo chanya.

“Unajua msimu uliopita haimaanishi kwamba kupoteza mbele ya Simba na Yanga hatukuwapeleka darasani hapana walituzidi uzoefu ila kwa sasa tumejipanga kuwarudisha darasani na matokeo tunachukua,” amesema Mwafulango

LihatTutupKomentar