BAADA ya Juma Abdul na Kelvin Yondani kumalizana na Yanga sasa kazi moja imebaki kumrejesha kikosini Andrew Vincent 'Dante'.
Abdul, Yondani na Dante ni mabeki ambao inaelezwa kuwa wapo kwenye mgogoro na mabosi wao kutokana na kutolipwa stahiki zao kwa muda mrefu.
Kwa sasa tayari Juma Abdul na Yondani wamerejea kikosini isipokuwa mchezaji mmoja tu ambaye ni Dante.
Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa anaamini mchezaji huyo atajiunga na timu itakaporejea kutoka kambini Kilimanjaro.
Fredrick Mwakalebela Makamu Mwenyekiti wa Yanga amesema kuwa mazungumzo yamefika sehemu nzuri na mchezaji huyo