Tetesi za Usajili Yanga leo 10 June 2019
Wakati Yanga ikiwa inaendelea na kazi ya kusajili baadhi ya nyota wapya na kuwaongezea wengine mikataba minono ili tu waweze kusalia Jangwani kwaajili ya msimu ujao
Inaelezwa kuwa Yanga imeshindwa kumalizana na Nyota wa KMC Ally Ally ambaye amekuwa moja ya nyota waliofanya vizuri ligi kuu soka ya Tanzania Bara TPL kwa msimu uliomalizika.
Ally Ally msomaji wa Kwataunit.co.ke ameeleza kuwa ni kweli alifanya mazungumzo na Yanga ya kuweza kumsajili lakini wameshindwana na Yanga kutokana na Dau yeye akitaka kiasi ambacho Yanga wameshindwa kumpatia.
Sasa Ally Ally ambaye alijiunga na KMC akitokea Stand United ya Shinyanga ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba na KMC Ya jijini Dar Es Salaam.