HAWA HAPA WQCHEZAJI WA YANGA MSIMU UJAO

YANGA wameamua kwamba mastaa wanne wa kigeni watakwenda na maji na kwenye usajili wao mpya watakuwa na nondo tisa mpya za kutoka nje ya nchi. Awali Kocha Mwinyi Zahera alitaka kusajili wachezaji sita tu wa kigeni ambao ni watu wa kazi watakaozama moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza lakini sasa ameamua kubadili gia
ili kujiweka fiti kwa Ligi ya Mabingwa Afrika wanayoanza mwezi Agosti.

Kocha Mwinyi Zahera

Uamuzi huo unamaanisha kwamba Papa Klaus Kindoki nje, Thabaan Kamusoko ‘Kampa kampa tena’ nje, Amissi Tambwe nje na Heritier Makambo yeye alishauzwa Horoya AC ya Guinea kwa mkataba wenye kipengele cha kuipatia Yanga asilimia 20 kila atakapouzwa siku zijazo. Kwenye upande wa wachezaji wazawa waliokuwa katika kikosi hicho msimu uliopita watabakia wachezaji nane tu.

Hiyo inamaanishwa kwamba Yanga itakuwa na kikosi cha wachezaji 21 wapya kabisa tayari kwa kuvaa uzi wa njano, kijani na nyeusi. Habari zinasema wachezaji hao ni Kelvin Yondani, Paul Godfrey, Fei Toto, Gadiel Michael, Juma Abdul, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Jafary Mohammed na Rafael Daud.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya Yanga ambazo Spoti Xtra limezipata ni kwamba, uongozi ulipanga kuwabakisha wachezaji wawili tu wa kigeni Tshishimbi na Kindoki lakini sasa umeamua kuwa utabikia na Tshishimbi peke yake.

Habari zinasema Kindoki wameamua kuachana nae na watampa stahiki zake kama wengine ili wapate nafasi ya kusajili majina mengine kujiweka sawa kimataifa. Awali Yanga walipanga kusalia na wachezaji wazawa 14 lakini wamekuna vichwa na kuona kuna ulazima wa kusaliwa na nane tu.

Mpaka sasa Yanga imeshafanya mazungumzo na kuelewana na wachezaji wapya 10, saba kati ya hao ni wa kigeni huku watatu wakiwa ni wazawa.

Kutokana na hali imebakiza nafasi mbili tu ili iweze kutimiza idadi ya wachezaji 10 wa kigeni kwa sababu moja inashikiliwa na Tshishimbi. Wapya wa kigeni ni Sadney Urikhob (Namibia), Issa Bigirimana (Rwanda), Maybin Kalengo (Zambia), Erick Rutanga (Burundi), Farouk Shikhalo (Kenya),
Lamine Moro (Ghana) pamoja na Patrick Sibomana (Rwanda).

Taarifa kutoka ndani ya uongozi ni kwamba, wameamua kuachana na Wakenya wawili ambao ni kiungo na winga wote wa Kariobangi Sharks baada ya vigogo wa klabu hiyo kutaka fedha nyingi kwa madai kuwa bado wana mikataba mirefu. Wazawa ni Abdul Aziz Makame (Zanzibar) pamoja na Ally Mtoni Sonso (Lipuli FC) huku ikiwa katika hatua za mwisho na kipa Metacha Mnata wa Mbao

LihatTutupKomentar