KAGERA SUGAR WAAPA KUENDELEZA UBABE

UONGOZI wa Kagera Sugar umesema kuwa hamna namna ya kuwazuia kubaki ndani ya Ligi Kuu msimu ujao kutokana na hasira walizonazo za kubaki ndani ya ligi  ili waendeleze ubabe wao kwa Simba kwa kuwatungua nje ndani.
Kagera Sugar ilishushwa kimakosa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kubaki daraja la kwanza kwa muda wa masaa machache kabla ya TFF kuamua kuwarejesha tena kwenye ligi wakiwa nafasi 18 ambayo ni lazima wacheze mchezo wa Playoff kupata nafasi ya kubaki ama kushuka.
Akizungumza na mkomesportnews Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa mchezo wao wa kwanza dhidi ya Pamba ugenini ulikuwa na ushindani walishindwa kupata matokeo hivyo watakaza mchezo wa marudio utakaopigwa Kaitaba.
"Mchezo wa kwanza tulishindwa kupata matokeo chanya sio mbaya tunajipanga kwa ajili ya mchezo wetu wa marudio, lengo letu lipo palepale kubaki kwenye ligi msimu ujao kwani uwezo tunao na mchezo wetu wa mwisho tutakuwa Kaitaba.
Kagera Sugar itamenyana na Pamba FC Juni 8 uwanja wa Kaitaba ukiwa ni mchezo wa marudio mshindi katika mchezo huo atapata nafasi ya kucheza ligi kuu
LihatTutupKomentar