Mtokea benchi kipindi cha pili, Quincy Promes akishangilia baada ya kuifungia Uholanzi bao la tatu dakika ya 114 katika ushindi wa 3-1 dhidi ya England usiku wa Jumatano katika mchezo wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mataifa ya Ulaya Uwanja wa Dom Afonso Henriques mjini Guimaraes. England ilitangulia kwa bao la penalti la Marcus Rashford dakika ya 32 baada ya yeye mwenyewe kuchezewa rafu na Matthijs de Ligt. Uholanzi ikazinduka kwa mabao ya Matthijs de Ligt dakika ya 73, Kyle Walker aliyejifunga dakika ya 97 baada ya kazi nzuri ya Promes aliyefunga bao la tatu. Sasa Uholanzi itakutana na Ureno katika fainali Juni 9, siku ambayo England itamenyana na Uswisi katika mchezo wa kuwania nafasi ya tatu