MSHAMBULIAJI WA TIMU YA TAIFA STARS AELEKEZA NGUVU ZOTE AFRICON

MSHAMBULIAJI wa timu ya soka ya Tanzania chini ya miaka 17, Serengeti Boys, Kelvin John maarufu Mbappe, amesema akili na mawazo yake yote ipo katika michuano ya Kombe la Afrika (AFCON).
Mbappe ni moja ya wachezaji waliyoitwa katika kikosi cha timu ya wakubwa Taifa Stars iliyoingia kambini kuanza maandalizi ya AFCON itakayoanza Juni 21 hadi Julai 19 mwaka huu nchini Misri.
Akizungumza nasi , Mbappe alisema kwake ni fahari kuitwa katika kikosi hicho akiwa pamoja na nyota wenye mafanikio.
“Kwangu ni mafanikio makubwa kuitwa na kujumuika na wachezaji kama Mbwana Samatta, Simon Msuva na wengine.
“Uwepo wao tu unanipa matumaini kuwa tuna kikosi bora na hivyo kujikuta natamani muda ufike ili twende Misri tukatimize majukumu yetu tukiwa na timu ya taifa,” alisema.
Mbappe aliwaomba Watanzania wawe na matumaini nao na kwamba hawatawaaangusha akiamini uwepo wa wachezaji wazoefu unaongeza chachu ya kwenda Misri na kufanya jambo zuri kwaajili ya nchi.

LihatTutupKomentar