YANGA YANASA SAINI YA MCHEZAJI HUYU KUTOKA SIMBA


Wakati msimu wa Ligi Kuu Bara ukielekea ukingoni, tetesi za wachezaji kuhama klabu moja kwenda nyingine zimezidi kushika kasi. 



Imeelezwa kuwa beki katili Lamine Moro raia wa Ghana aliyeichezea klabu ya Simba kwenye michuano ya Sportpesa Cup amewashatua Dar kumalizana na Yanga. 

Moro alikuwa na Simba katika mashindano hayo ya SportPesa ikiwa ni sehemu yake ya majaribio. 

Licha ya kucheza, Simba haikuonekana kuwa na nia naye na badala yake aliachwa akarejea kwao bila kupata mkataba

LihatTutupKomentar