JUNI 2 mwaka huu, uwanja wa Taifa, nahodha wa timu ya Tanzania, 'Taifa Stars' atashuka uwanjani kumenyana na msanii wa muziki wa kizazi kipya na mshambuliaji wa Coastal Union
Mechi hiyo ni ya hisani kwa timu hizo mbili ni maalumu kwa ajili ya kuwachangia vijana wanaoishi mazingira magumu pamoja na kutoa misaada kwenye shule.
Ofisa Habari wa timu ya Samatta, Haji Manara amesema kuwa mchezo huo utakuwa ni maaalumu kwa ajili ya kumpongeza nahodha kwa kutimiza wajibu wake kwenye timu ya KRC Genk ya Ubelgiji kwa kutwaa kombe na kuwaaga wachezaji wa timu ya taifa.
“Samatta ataingia nchini May 25 mwaka huu akitokea Maka ambako ataenda kwa ajili ya hija na baada ya hapo atakuja kuanza maandalizi ya mchezo huo kwa kufanya ziara kwenye vyombo mbalimbali vya Habari.
“Mbali na hilo pia siku hiyo ya Juni 2 baada ya mchezo atakuwa na Iftari ambayo itafanyika Serena Hoteli mjini Posta ikijumuisha wachezaji wote wa mchezo huo,” amesema Manara.
Ofisa Habari wa timu Kiba, Sud Brown amesema kuwa wapo bega kwa bega kumpongeza Samatta kutwaa kombe pamoja na kurudisha kwa jamii kile walichokipata ila kichapo hakikwepeki.
"Kumpiga bingwa ni raha hivyo safari hii tumejipanga kufanya kweli kwenye mchezo huo huku tukimpongeza kwa mtindo wa kipekee," amesema