MKUDE ATOA MSAADA KWA MCHEZAJI HUYU WA YANGA


Mchezaji wa klabu ya Simba na timu ya taifa ya Tanzania, Jonas Mkude, ametoa fedha taslimu shilingi laki tano kumsaidia mchezaji wa zamani wa Pamba ya Mwanza na Simba, Alphonce Modest kwa ajili ya matibabu. 



Modest ambaye amezichezea pia timu za Yanga na Mtibwa Sugar, amekuwa akisumbuliwa na homa kwa muda mrefu. 

Pia wachezaji wa zamani kupitia chama chao wametoa shilingi laki saba kumchangia mwenzao. 

Fedha hizo zimekabidhiwa kwa baba yake Modest, mitaa ya Kinondoni jijini Dar Es Salaam. 

Pichani juu Mkude anaonekana akiwa na baadhi ya wachezaji wa zamani; Mohamed Mkweche, Shaban Katwila, Athanas Michael, Mwenyekiti Paul Lusozi na Katibu Sebastian Mwendamaka
LihatTutupKomentar