MECHI MOJA LIGI KUU TANZANIA BARA YASOGEZWA MBELE


Ligi kuu iliendelea leo kwa mchezo kati ya Singida United dhidi ya Ruvu Shooting na mechi hiyo ilimalizika kwa Singida United kubanwa na Ruvu Shooting mara baada ya Suluhu ya bila kufungana.

Kesho kulitakiwa kuchezwa mechi 2 moja kati ya African Lyon dhidi ya Tanzania Prisons na nyingine kati ya Azam Fc dhidi ya JKT Tanzania.

Mechi kati ya Azam Fc dhidi ya JKT Tanzania imebaki palepale na itachezwa saa moja usiku uwanja wa Azam Complex wakati mchezo kati ya African lyon dhidi ya Tanzania Prisons ukisogezwa mbele mpaka jumamosi kutokana na Uwanja wa Uhuru kuwa na matumizi mengine

LihatTutupKomentar