TANZIA :KLAUS KINDOKI AFIWA NA BABA YAKE

Mlinda lango wa klabu ya Yanga Klaus Kindoki amepata msiba wa kufiwa na Baba yake mzazi aliyefariki dunia nchini Congo

Kulingana na taarifa iliyotolewa na uongozi wa Yanga, mazishi yatafanyika huko huko Congo Jumapili Januari 20 2019

Tunampa pole sana Kindoki, Mwenye ez Mungu amtie nguvu katika kipindi hiki cha majonzi
Msiba huo ni pigo kwa Yanga kwani Kindoki alitarajiwa kukaa langoni kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Stand United.

Mlinda lango aliyetua Yanga wakati wa usajili wa dirisha dogo Ibrahim Hamid huenda akapata nafasi ya kucheza mchezo wake wa kwanza kwenye ligi kuu ya Tanzania Bara

LihatTutupKomentar