KOCHA YANGA WAFUNGUKA TIMU ZINAZO MNYIMA USINGIZI


Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa ni timu mbili pekee ambazo zinaweza kuwazuia kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Akifanya mahojiano na Uhai FM pamoja na Azam TV, Zahera ameeleza timu zote hizo zina nafasi ya kutwaa ubingwa.

Kocha huyo amezitaja timu hizo kuwa ni Simba na Azam ambazo zina vikosi viwili vyenye uwezo wa kila mmoja kutwaa taji la ligi msimu huu.

Kwa upande wa Simba Zahera amesema timu hiyo ina takribani mechi tatu mkononi ikicheza michezo 14 pekee wakati wao wakiwa wamechaza 17.

Aidha kwa upande wa Azam mpaka sasa wako nafasi ya 2 wakiwa na alama 40 huku Yanga wakiwa 47.

Aidha, Zahera amesema licha ya msimamo kuonesha wao wako juu, bado mpaka sasa kuna mechi nyingi hazijachezwa hivyo kila timu pale kati ya Azam, Yanga na Simba ina nafasi ya kubeba taji

LihatTutupKomentar