YANGA WAFUNGUKA HAYA KWA WANACHAMA WAKE

Habari njema kutoka Yanga leo asubuhi 27.12.2018

Klabu ya Yanga December 29 itakuwa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City mechi hiyo ikipangwa kuchezwa katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya .

Awali Yanga kupitia kwa viongozi wake na Kocha wake mkuu uliwataka washabiki na wanachama wa Yanga kuichangia timu yao ili iweze kusafiri kwa ndege mpaka mkoani Mbeya.

Habari njema ikufikie tu kuwa Kikosi cha Yanga leo asubuhi kimeondoka kwa ndege kwenda mkoani Mbeya kwaajili ya pambano lao dhidi ya Mbeya City huku kocha Mwinyi Zahera naye akiwa ameshatua nchini na ataongozana na Kikosi cha Yanga.

Kocha wa Yanga  baada ya kufanikishiwa zoezi la Usafiri wa ndege amewashukuru wote waliyoichangia timu yao.

“Tunawashukuru sana mashabiki na wanachama wetu kwa msaada wao kwetu sisi tunawaahidi kuwapa furaha ya ushindi kwenye kila mchezo utakao kuwa mbele yetu Mungu atusaidie sana na awabariki wote

LihatTutupKomentar