TETESI ZA USAJIRI ULAYA LEO IJUMAA


 

Tetesi za usajili barani ulaya leo Ijumaa 7.12.2018

Beki wa kulia wa Manchester United Antonio Valencia, 33, huenda akajisajiliwa na West Ham msimu ujao. (Sun)

Meneja wa Derby Frank Lampard amethibitisha kuwa Liverpool wanaweza kumchukua mshambuliaji wao wa zamani Harry Wilsoncan, 21, ambaye amekuwa akiichezea Derby kwa mkopo kufikia Januari. (Talksport)

Fulham wanapania kumsajili mlinzi wa Manchester United Matteo Darmian, 29, lakini kiungo huyo anatafakari kurudi nyumbani, kuna tetesi kuwa Inter Milan na Lazio wanammezea mate. (Tuttomercato, via Talksport)

Wolves wanajiandaa kumpatia ofa ya euro milioni 17 winga wa Japan Shoya Nakajima,24, kutoka klabu ya Portimonense ya Ureno. (Daily Mail)

Meneja wa Newcastle boss Rafael Benitez anaazimia kumsajili mshambuliaji wa Atlanta United Miguel Almiron, 24, na huenda kiungo huyo akaichezea Newcastle kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Barcelona Denis Suarez, 24, huenda akahama klabu hiyo endapo hatajumuishwa katika kikosi cha kwanza mara kwa mara.

 

Chelsea na AC Milan ni miongoni mwa vilabu vikubwa vinavyopigiwa upatu kumsajili. (Calciomercato via Daily Star

Newcastle United wanafuatilia mchezo wa mshambuliaji wa zamani wa Sunderland forward Fabio Borini, mwenye umri wa miaka 27.

Kuna tetesi kuwa klabu hiyo huenda ikaweka dau la kumnunua mwezi Januari iwapo mchezaji huyo anataka kuhama AC Milan. (Tuttomercato, via Sunderland Echo)

Danny Rose amesema heshima ya kucheza katika uga wa Wembley haipo tena baada ya Tottenham kurekodi idadi ndogo ya mashabiki waliyokuja kushangilia mechi yao dhidi ya southampton siku ya Jumatano. (Evening Standard)

Kiungo wa Ajax, Frenkie de Jong, 21, ambaye anapigiwa upatu kujiunga na Manchester City, amekataa kuthibitisha tetesi kuwa huenda akahama klabu hiyo msimu huu wa joto. (Manchester Evening News)

 

Jack Grealish,23, anayechezea Aston Villa, amesema “hainisumbui kabisa” alipogusiwa pendekezo la kuhamia Tottenham msimu ujao. (Sky Sports)

Mpango wa Rangers kusalia na mlinzi Joe Worrall kwa mkopo zimepigwa zitafaulu baada ya meneja wa Nottingham Forest boss Aitor Karanka kuthibitisha kuwa hamchukua hadi pale mchezaji huyo atakapotoa ombi la kururidi nyumbani. (Daily Record)

Mlinzi wa Juventus Alex Sandro, ambaye amehusishwa na tetesi za kuhamia Manchester United mwezi Januari mwakani, yuko karibu kuafikiana kwa mkataba mwingine na mabigwa hao wa ligi ya Italia. (Goal)

Kiungo wa kati wa Manchester United Jesse Lingard amethibitisha jinsi walivyopata uchovu baada ya kuiwakilisha Englanda katika michuano ya kombe la dunia. (Telegraph)

LihatTutupKomentar