MWENYEKITI YANGA AFUNGUKA MENGI HAYA HAPA


Mwenyekiti wa Matawi Yanga ukanda wa Temeke, Mustapha Mohammed ameibuka na kupinga kauli ya kikosi cha Yanga kilinyimwa nafasi ya kufanya vizuri katika msimu wa Ligi. 

Mohammed amesema Yanga inajiamini kutokana na kuwa na rasilimali watu na wana kikosi cha wachezaji ambao wanajali kujituma zaidi. 

Mwenyekiti huyo pia amesema kwa namna wanayanga walivyojiweka pamoja inasaidia timu yao kwenda vema kwa kuwa wamejitoa katika kuichangia klabu kulingana na namna hali ya uchumi ilivyo hivi sasa. 

Yanga mpaka sasa haijapoteza mchezo wowote kwenye ligi zaidi ya kwenda sare mara mbili dhidi ya Ndanda FC. na Simba SC

Kutokana na kuwa hawajapoteza mchezo hata mmoja, Mohammed amewataka wale wote wanaidharau Yanga ikiwemo baadhi ya mashabiki wa Simba kujipanga vema kwani wanazidi kupambana kimyakimya. 

Na katika msimamo wa ligi kikosi hicho kimeshikilia usukani wa ligi kwa kuwa na alama 44 kikiwa kimecheza jumla ya michezo 16. 

LihatTutupKomentar